Straika Mrundi wa Yanga, Amissi Tambwe aliyekuwa majeruhi kwa kipindi kirefu ameibuka na kufunguka kuwa amerejea kwenye makali yake.
Tambwe ambaye alikuwa nje kutokana na kusumbuliwa na goti lililomfanya akose mechi 11 za timu hiyo za ligi kwa mara ya kwanza Jumapili iliyopita alionekana uwanjani kwenye mchezo wa timu hiyo wa Kombe la Shirikisho (FA) dhidi ya Reha ambapo alihusika kwa kufunga bao moja katika ushindi wa mabao 2-0.
Mfungaji huyo wa Ligi Kuu Bara, mara mbili amesema mara baada ya kuonekana tena uwanja kwa sasa mtihani wa kwanza kwake ni kuhakikisha Yanga inakuwa na matokeo mazuri katika kila mchezo wake pamoja na kufunga mabao mengi tofauti na ilivyokuwa kwenye baadhi ya mechi.
“Nashukuru kwamba nimerejea ndani ya timu baada ya kupita kwa muda mrefu nikiwa nje kutokana na majeraha, na pia jambo la kushukuru ni kuwa nimeingia na kuiwezesha timu kupata matokeo kwenye mechi yetu iliyopita tena nikifunga na bao.
“Jambo ambalo lipo mbele yangu kwa sasa ni kuona kwamba Yanga inafanya vizuri kwenye kila mechi ya michuano tena na mimi nikiwa nafunga mabao, naamini yote hayo yatawezekana kwa sababu ya ushirikiano ambao nimeupata kwa wenzake mara baada ya kurejea tena uwanjani,” alisema mshambuliaji huyo.
No comments:
Post a Comment