Friday 8 December 2017

Cristiano Ronaldo amshinda Messi atwaa tuzo ya Ballon D'or.

'Of course, I feel happy. It's a big moment in my career,' Ronaldo said upon being presented with the award for the fifth time
Mshambuliaji wa klabu ya Real Madrid, Mreno Cristiano Ronaldo ametwaa tuzo ya Ballon d'Or kwa mwaka wa pili mfululizo usiku wa kuamkia leo.

Ronaldo amemshinda mpinzani wake wa karibu Lionel Messi, katika tuzo hiyo na kuweza kuitwaa kwa mara ya tano na kuwa sawa na Messi ambae pia ametwaa kwa mara tano.
Nyota wa Barcelona Lionel Messi, amepata nafasi ya pili huku mchezaji mahiri wa Psg ya nchi Ufaransa Neymar Jr,akiwa katika nafasi ya tatu
 Ronaldo also showed his lighthearted side, joking about wanting seven children when asked for his Christmas wishlist
Msimu uliopita Ronaldo aliisaidia timu yake ya Real Madrid kutwaa ubingwa wa klabu bingwa barani Ulaya na ubingwa wa la Liga kwa mara ya kwanza toka toka mwaka 2012.
(L-R top-bottom) Ronaldo with his 2008, 2013, 2015, 2016 and (main photo) holding the 2017 Ballon d'Or award in Paris
Picha za C.Ronaldo akiwa na Ballon d'Or 2008, 2013, 2015, 2016 na Picha kubwa ni ya  2017

Ballon d'Or ni tuzo ambayo imekua ikitolewa na jarida la nchini Ufaransa toka mwaka 1956 na kura hupigwa na waandishi wa habari wapatao 173, duniani kote

No comments:

Post a Comment