Wednesday 13 December 2017

Hizi ndio Timu zilizopangiwa Simba na Yanga katika michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Image result for simba na yanga katika ngao ya jamii 2017
Ratiba ya Kombe la Shirikisho Afrika imetoka na Simba imepata bahati ya kupangwa na timu laini au kibonde kutoka Djibouti.

Simba imepangwa kuanza Gendamarie, timu ambayo imekuwa ni moja ya vibonde katika michuano ya Kagame ambayo ni maalum kwa ukanda wa Afrika Mashariki na Kati.


Hata hivyo Shirikisho la Soka Afrika (Caf), limeipangia Yanga kuanza na St Louis ya Shelisheli, timu ambayo hauwezi kusema ni mlima mrefu kwa kwa Yanga.


Ingawa Yanga watapaswa kuwa makini kwa kuwa ni soka na soka la Shelisheli limekuwa likipanda, lakini haiwezi kuwa kazi itakayowashinda wakiamua “lazima” wasonge mbele.

No comments:

Post a Comment