Tuesday 12 December 2017

Kenya yaadhimisha kumbukumbu ya miaka 54 ya Uhuru Leo.

Image result for uhuru kenyatta in independent day
Kwa mara ya kwanza sherehe za maadhimisho ya tarehe 12 Disemba, siku kuu ambayo Kenya ilijipatia uhuru, zitafanyika katika uwanja wa Kimataifa wa Michezo wa Moi Kasarani, Jumanne Disemba 12 mwaka huu wa 2017.

Wakenya wameanza kumiminika katika uwanja huo ulioko katika maeneo ya barabara kuu ya Thika, kilomita 10 kutoka katikati mwa mji mkuu Nairobi, huku usalama ukiimarishwa.
Maadhimisho hayo ya 54 tangu Kenya ilipojipatia Uhuru wake mwaka 1963, yataongozwa na Rais Uhuru Kenyatta.
Sherehe hizo zitashuhudia, utumbuizaji wa kila aina, ukiwemo nyimbo za kitamaduni na dini, michezo ya kuigiza, mchezo wa kwata, na maonyesho ya ndege za kijeshi pamoja na gwaride maalum ya vikosi vyote vya usalama.
Kwa mjibu wa msemaji wa Serikali Eric Kiraithe, milango ya uwanja huo wa Kasarani itafunguliwa saa moja kamili asubuhi, ili kuwakubalia raia pamoja na watu mashuhuri kuingia tayari kwa sherehe hizo ambazo zitaanza muda mfupi baada ya saa nne mchana.
Sherehe hii ni muhimu kwa Rais Uhuru Kenyatta ambaye aliapishwa majuma mawili yaliyopita kuchjukua hatamu ya miaka mitano ya muhula wake wa pili na wa mwisho uongozini, baada ya kushinda kwenye uchaguzi tata ambao uliosusiwa na upinzani mnamo Oktoba 26.

No comments:

Post a Comment