Monday, 4 December 2017

Kiungo wa Yanga Tshishimbi aanza kufanya Mazoezi Mepesi.


Image result for tshishimbi yanga
KIUNGO wa Yanga, raia wa Dr Congo, Kabamba Tshishimbi, yupo fiti na huenda akaanza mazoezi mepesi ya gym leo asubuhi.


Mkongo huyo alikuwa nje kwa muda wa wiki moja na nusu akiuguza majeraha ya kifundo cha mguu aliyoyapata wakati timu hiyo ikijiandaa na mechi dhidi ya Mbeya City.

Timu hiyo, itaanza mazoezi yake leo baada ya kumaliza mapumziko ya wiki moja waliyopewa na Kocha Mkuu wa timu hiyo, Mzambia, George Lwandamina.

Daktari Mkuu wa timu hiyo, Edward Bavo, alisema kiungo huyo yupo fiti hivi sasa na huenda akawepo kwenye orodha ya wachezaji watakaoivaa Mbao FC.

No comments:

Post a Comment