Sunday, 17 December 2017

Maamuzi ya Yanga kuhusu Viungo wake Kamusoko na Papy Tshishimbi.

Image result for Kamusoko na Papy Tshishimbi
Yanga imekuwa ikifanya juhudi kubwa za makusudi kuhakikisha inawarejesha mtamboni viungo wake wawili, Thabani Kamusoko na Papy Tshishimbi.

Viungo hao, wote walikuwa majeruhi licha ya kuanza mazoezi taratibu, Tshishimbi ndiye anaonekana kuimarika zaidi.

Lakini taarifa zinaeleza, Kocha George Lwandamina amesisitiza kutaka kuona wanarejea.

"Kocha ametaka usimamizi wa karibu kwao kuhakikisha wanarejea," kilieleza chanzo.

"Ameisisitiza kila kitu kiende sahihi, wao wafuate wanachotakiwa kufanya ikiwemo mazoezi mapemesi na kadhalika."

Yanga inapowatumia viungo hao, Lwandamina amekuwa na uhakika katika eneo la kiungo. Lakini alikuwa akilazimika kuwatumia vijana kama Pius Buswita, Raphael Daud baada ya wakongwe hao kuwa majeruhi.

No comments:

Post a Comment