Monday, 18 December 2017

Tetesi zote za Soka kutoka barani Ulaya Jumatatu Disemba 18.

Related image
Pierre-Emerick Aubameyang
Manchester United wanatarajiwa kuwasilisha ofa ya £60m kutaka kumnunua beki wa Juventus Alex Sandro, 26, mwezi Januari. (Mirror)

Rais wa Barcelona naye alikutana na familia ya Antoine Griezmann katika juhudi za karibuni zaidi za klabu hiyo kutaka kumnunua mshambuliaji huyo wa Atletico Madrid mwenye miaka 25. (Mundo Deportivo)
Chelsea nao wanamnyatia mshambuliaji wa Crystal Palace Wilfried Zaha, 25, na wanataka kumchukua Januari. (Mirror)
The Blues wako tayari kumuuza beki wao wa kati kutoka Brazil David Luiz ambaye kwa sasa ana miaka 30. (Mirror)
Mabingwa wa Italia Juventus pamoja na wenzao wa Uhispania Real Madrid ni miongoni mwa klabu ambazo zina hamu sana ya kumchukua Luiz. (Daily Mail)
Alex SandroHaki miliki ya picha
Image captionBeki wa Brazil Alex Sandro
Mshambuliaji wa Arsenal Alexis Sanchez, 28, amekataa mshahara wa £400,000 kila wiki kutoka kwa klabu moja ya China kwa sababu anataka sana kuhamia Manchester City. (Sun)
Everton nao waliwatuma maskauti kumfuatilia beki kinda wa Charlton Ezri Konsa, 20, Jumamosi. (Liverpool Echo)
Bayern Munich wameafikiana mkataba wa euro 15m (£13.2m) kumchukua mshambuliaji wa Hoffenheim Sandro Wagner, 30, mwezi Januari. (Bild)
Wamiliki wa Stoke wametiwa wasiwasi sana na matokeo mabaya ya klabu hiyo karibuni lakini bado wanaamini Mark Hughes anafaa kusalia kama meneja wao. (Stoke Sentinel)
Liverpool hawatawasilisha dau kumtaka beki Virgil van Dijk iwapo Southampton hawatashusha thamani ya Mholanzi huyo wa miaka 26 ke kutoka £70m. (Irish Independent)
Virgil van DijkHaki miliki ya picha
Kiungo wa kati wa Swansea na mkufunzi msaidizi Leon Britton, 35, atachukua usukani kama meneja iwapo Paul Clement atafutwa. (Sun)
Nyota wa Real Madrid Cristiano Ronaldo, 32, anataka aongezewe mshahara wake na kuwa mchezaji anayelipwa pesa nyingi zaidi duniani. (Marca)
Kiungo wa kati wa zamani wa Manchester United Bastian Schweinsteiger, 33, amepokea ofa kutoka kwa klabu kadha za Bundesliga huku mkataba wake klabu ya MLS ya Chicago Fire ukitarajiwa kufikia kikomo. (Die Welt)
Mshambuliaji wa Borussia Dortmund Pierre-Emerick Aubameyang aliongeza mkataba wake kisiri katika klabu hiyo kwa mwaka mwingine mmoja hadi mwaka 2021. (Kicker)
RonaldoHaki miliki ya picha
Cristiano Ronaldo anataka wachezaji wa Barcelona waandalie klabu ya Real Madrid gwaride la heshima klabu hizo zitakapokutana katika El Clasico Jumamosi. (Marca)

No comments:

Post a Comment