Thursday, 7 December 2017

Tetesi zote za Soka kutoka Ulaya hii leo Alhamisi.

Image result for Eden Hazard
Meneja wa Real Madrid Zinedine Zidane na rais Florentino Perez wamewasiliana na mchezaji wa Chelsea Eden Hazard, 26. (Diario Gol via Daily Mail)

Mlinzi wa West Brom Jonny Evans, 29, anatafuwa na Everton na West Ham huku Manchester United nayo ikiwa inammezea mate. (Daily Mirror)
Juan MataHaki miliki ya picha
Image captionJuan Mata
Manchester United wamemsalimisha mchezaji Juan Mata , 29, kwa Inter Milan kama makubaliano ya kumleta mchezaji wa safu ya kati Joao Mario, 24. (Corriere dello Sport - in Italian)
Manchester City na Liverpool wote wanamtaka mchezaji wa kiungo cha kati wa Nice Jean Seri , 26, ambaye pia anatazamwa na Barcelona. (Daily Mail)
David MoyesHaki miliki ya picha
Image captionDavid Moyes
Maajenti wa Southampton wamekuwa wakimtazama wing'a wa Basel Mohamed Elyounoussi, 23. (Blick - in German)
Meneja wa West Ham David Moyes anatathmini kumwacha nje kipa Joe Hart, 30, wakati wa mechi ya Jumamosi na Chelsea. (Guardian)
Mshambuliaji wa Bolton Wanderers Gary Madine, 27, ni kati ya wachezaji wanaowindwa na Sunderland mwezi Januari. (Sunderland Echo)
NeymarHaki miliki ya picha
Image captionNeymar
Mashabiki wa Bayern Munich walichapisha pesa bandia za noti ya euro 500 zenye picha ya Neymar na kumrushia mchezaji huyo mbrazil wakayt wa ushindi wao dhidi ya Paris St-Germain.
Lionel Messi amekataa ofa ya pauni 850,000 kwa wiki kutoka Manchester City kabla ya kusaini mkataba mpya na Barcelona. (Marca - in Spanish)

No comments:

Post a Comment