Friday, 5 January 2018

Ahadi ya Straika wa Mbao FC Habibu kuhusu mpango wa kumpoteza Okwi Ligi kuu.

Image result for Habibu Kiyombo wa Mbao FC
Siku chache baada ya kufanikiwa kuiua Yanga kwa mara nyingine, mshambuliaji wa Mbao FC, Habibu Haji Kyombo ametamba kuwa anataka kufunga mabao zaidi ya 15 kwenye Ligi Kuu Bara.

Hadi sasa Mganda wa Simba, Emmanuel Okwi ndiye anayeongoza kwa mabao katika ligi hiyo akiwa amefunga mabao nane huyu Kiyombo akiwa na mabao saba. Hivyo, kwa kauli hiyo Okwi anatakiwa kujipanga vizuri.

Kyombo alisema amejitosa  kupambana na kuweza kufunga mabao mengi zaidi tofauti na msimu uliopita. 

“Ndiyo maana najituma kwa bidii na kushirikiana na wenzangu ili kuhakikisha tunaisaidia timu yetu kupata matokeo ambayo ni kufunga mabao mengi bila kujali hii ni timu gani,” alisema Kiyombo ambaye msimu uliopita alifunga mabao manne.

Wakati huohuo, inadaiwa kuwa uongozi wa Yanga umeanza mikakati  ya kutaka kumsajili Kiyombo kwa ajili ya msimu ujao ili kuchukua nafasi ya Mzimbabwe, Donald Ngoma ambaye amekuwa msumbufu kwao.

“Tumemfuatilia sana mchezaji huyo na tumegundua kuwa atatusaidia kuondokana na usumbufu huu ambao tumekuwa tukiupata kutoka kwa wachezaji wa kimataifa. 

“Kila mtu anajua ni jinsi gani wanatusumbua, mfano  mzuri ni Donald Ngoma, kwa hiyo endapo tutamsajili Kiyombo basi atatusaidia kupunguza usumbufu huu ambao tunaupata hivi sasa,” kilisema chanzo hicho cha habari.

Alipoulizwa kuhusiana na hilo Katibu Mkuu wa Yanga, Charles Mkwasa hakutaka kusema chochote kuhusiana na hilo lakini kwa upande wake Kiyombo alipoulizwa, alisema: “Kwa sasa akili yangu ipo katika kuisaidia Mbao kwa hiyo kama Yanga wananitaka wasubiri ligi iishe kwanza.” 

No comments:

Post a Comment