Baada ya kukaa nje kwa zaidi ya mwezi mmoja, hatimaye kiungo mwenye kasi wa Simba, Emmanuel Okwi anaanza mazoezi leo.
Okwi aliyejiunga na kambi ya Simba iliyo mjini Morogoro akitokea kwao Uganda, anaanza mazoezi na wenzake leo.
Kocha Masoud Djuma ambaye alimtaka Okwi kubaki Uganda hadi atakaporejea, amempokea vizuri na kutoa ruhusa ya leo kuanza kazi na wenzake.
Okwi ndiye kinara wa ufungaji mabao Ligi Kuu Bara msimu huu akiwa na mabao nane licha ya kuwa nje ya kikosi kwa muda mrefu.
Awali ilielezwa kwamba alitaka kurejea nchini lakini Kocha Masoud Djuma akamtaka kubaki Uganda.
No comments:
Post a Comment