Thursday 25 January 2018

Halima Mdee atuma ujumbe kwa Jaji Mkuu kuhusu kesi ya Sugu.

Image result for Halima Mdee
Mbunge wa jimbo la Kawe (CHADEMA) Halima Mdee amefunguka na kumuomba Jaji Mkuu Prof. Ibrahim Hamis Juma kufuatilia mwenendo wa kesi za kisiasa nchini na kudai kuwa baadhi ya mahakimu wamekuwa wakipindisha mambo kwa sababu za kisiasa.

Halima Mdee amesema hayo wakati akiongea na kituo cha EATV na kusema kuwa Jaji Mkuu anaposema wanasiasa wasiingilie Mahakama hivyo na yeye anapaswa kusimama na kuhakikisha kuwa Mahakimu wakitenda haki na kukemea wale ambao kwa makusudi wamekuwa wakipindisha haki za watu.

"Ni zaidi ya wiki sasa Mhe. Sugu yupo ndani lakini amenyimwa dhamana kwa kosa ambalo linadhaminika kisheria na kiutaratibu kwa mujibu wa sheria zetu kama kosa linadhaminika ni wajibu wa polisi kutoa dhamana na polisi wakikushikilia ndani ya zile saa 48 wakikupeleka mahakamani ni jukumu la Mahakama kufanya hivyo sasa suala la Sugu limeenda Mahakamani ambapo huo ndiyo muhimili pekee ambao tunautegemea .

"Sasa unapokwenda Mahakamani sehemu pekee ambayo unaitegemea kupata haki halafu unaona hiyo haki haipatikani kwa makusudi kabisa hivyo Jaji Mkuu na yeye anapaswa kuyatambua haya na kuwakemea baadhi ya Mahakimu ambao wanafanya vitu kama hivi" alisema Mdee

Mbali na hilo Halima Mdee amedai kuwa kuna tetesi za kutaka kumfunga Mbunge wa Mbeya Mjini Mhe. Joseph Mbilinyi “Sugu' kama ambavyo alifungwa Mbunge wa Kilombero, Peter Lijualikali.

No comments:

Post a Comment