Pamoja na Simba kuitwanga Majimaji kwa mabao 4-0, Kocha Pierre Lechantre amesema anataka mabao zaidi.
Raia huyo wa Ufaransa anaamini timu yake ina uwezo wa kufunga mabao zaidi ya hayo waliyofikia.
“Kocha amesema mabao manne ni jambo zuri lakini sasa anataka mabao zaidi,” kilieleza chanzo.
“Uzuri wake ni muelewa na anasikiliza, Kocha Masoud pia yuko hivyo kwa hiyo tunaamini tunaweza kufanya vizuri zaidi.”
Simba imefanikiwa kufunga mabao 12 katika mechi nne, hali inayoifanya kuwa ndiyo hatari zaidi katika kipindi hiki.
Kocha huyo alikuwa akiiongoza Simba katika mechi yake ya kwanza na kufanikiwa na kuibuka na ushindi huo.
No comments:
Post a Comment