Friday, 26 January 2018

Majimaji FC wazungumzia mchezo wao na Simba.

Image result for Majimaji FC
Benchi la Ufundi la Majimaji FC limesema kuwa, kuelekea mchezo wao wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Simba, hawawaogopi wapinzani wao hao na hawatafanya mzaha kwani wamejipanga kuondoka na pointi tatu.

Majimaji inayodhaminiwa na Kampuni ya Kubashiri Matokeo ya Sokabet, keshokutwa Jumapili itapambana na vinara wa ligi hiyo Simba kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara utakaopigwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar.

 Ofisa Habari wa Majimaji, Onesmo Ndunguru alisema: “Leo  tumeanza safari ya kuja Dar ambapo tukifika tutapumzika  kisha Jumamosi tutafanya mazoezi ya mwisho kabla ya mchezo wenyewe Jumapili.

“Tunafahamu kwamba mchezo uliopo mbele yetu ni mgumu, hivyo maandalizi yalianza tangu tulipomaliza mechi yetu na Singida United, Jumatatu iliyopita.

“Hatutakuwa tayari kuona tunapoteza mchezo huo kwani kwa jinsi ligi ilivyo, ukipoteza mechi moja tu basi upo sehemu mbaya ndiyo maana tunakuja kucheza na Simba na nafasi tuliyopo hatutakiwi kufanya mzaha.”

No comments:

Post a Comment