Monday 15 January 2018

Pascal Haonga (CHADEMA):Hawatumii akili bali wanatumia matope.

Image result for Pascal Haonga
Mbunge  wa Jimbo la Mbozi (Chadema), mkoani Songwe, Pascal Haonga, amejitabiria mabaya baada ya kuwataka wananchi kuchoma nyumba yake iwapo atahamia Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Haonge amewataka wananchi hao kufanya hivyo kutokana na baadhi ya viongozi wa upinzani hususan madiwani na wabunge kujiuzulu na kuhama vyama vyao.

Idadi kubwa ya madiwani wa upinzani wamejiuzulu na kuhama vyama vyao na kujiunga na CCM wakati wabunge watatu hadi sasa wamejiuzulu na kuhama vyama vyao ambao ni Godwin Mollel (Siha-Chadema) aliyehamia CCM, Lazaro Nyalandu (Singida Kaskazini-CCM) aliyehamia Chadema na Maulid Mtulia (Kinondoni-CUF) aliyejiuzulu na kujiunga na CCM.

Haonga alitoa maelekezo hayo Jumamosi alipowahutubia wananchi wa Mji wa Mlowo wilayani Mbozi, ambapo alisema hawezi kuwasaliti wananchi waliosimama kidete kipindi cha Uchaguzi Mkuu wa 2015 kuhakikisha anapata ushindi.

Alisema wakati wa uchaguzi kulikuwa na matukio ya vurugu katika jimbo hilo huku baadhi ya watu wakipoteza biashara zao, kujeruhiwa na wengine waliwekwa ndani kwa ajili ya kupigania ushindi wake na wa Chadema, hivyo hawezi kuwasailiti.

Aliwaponda baadhi ya wabunge na madiwani wa chama hicho na vyama vingine vya upinzani wanaohamia CCM kwa madai ya kuunga mkono Serikali ya awamu ya tano kuwa hawatumii akili bali wanatumia matope.

“Najua baada ya baadhi ya wasio na msimamo kuanza kuhamia CCM, mmepata hofu kuwa hata kwangu itakuwa hivyo, niwahakikishie mimi siwezi kulamba matapishi yangu, kuna watu mlipigwa mabomu ya machozi, kuna watu walifungwa na kuna wengine walijeruhiwa kuhakikisha tunashinda, ikitokea hivyo kateketezeni nyumba yangu,” alisema Haonga.


No comments:

Post a Comment