Wednesday 28 February 2018

Akilimali azidi kumuaribia Golikipa wa Yanga Rostand afunguka mengine.


Katibu wa Baraza la Wazee wa Yanga, Ibrahim Akilimali, ameendelea kutoa msisitizo wake kuwa bado hampi nafasi Golikipa Youthe Rostand kuendelea kusalia langoni.


Akilimali amesema uimara wa kipa huyo umepotea kutokana na hivi karibuni kiwango chake kushuka hivyo si wakati mwafaka wa kuendelea kumtumia.

Aidha Akilimali ameeleza ifikie wakati sasa benchi la ufundi limpe nafasi Beno Kakolanya na Ramadhan Kabwili ya kucheza kuliko kuendelea kusalia benchi.

"Mimi nimeona ameshuka kiwango chake kwa muda mrefu sasa, sioni haja ya kuendelea kuwa kipa katika klabu yetu, nadhani ifike hatua sasa vijana Ramadhan Kabwili na Beno Kakolanya wapewe nafasi ya kucheza nafasi yake" amesema Akilimali.

Yanga ipo mkoani Mtwara leo kucheza dhidi ya Ndanda FC, mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

No comments:

Post a Comment