Wednesday 21 February 2018

Amissi Tambwe awatoa hofu mashabiki wa Yanga.

Image result for amisi tambwe
KIKOSI cha Yanga, leo Jumatano kinashuka uwanjani kupambana na St Louis ya Shelisheli katika mchezo wa marudiano wa Klabu Bingwa Afrika, huku kikiwakosa nyota wake wanne wa kigeni kutokana na majeraha


Kwenye mchezo huo muhimu, Yanga itamkosa, Obrey Chirwa, Amissi Tambwe, Donald Ngoma pamoja na Thaban Kamusoko.

“Yanga hawana haja ya kuwa na wasiwasi na wache­zaji watakaocheza dhidi ya St Louis, kwani ni wacheza wa­zuri na wenye uwezo kufanya vizuri endapo wataamua kupambana.


“Nasema hivyo kwa sababu ninawajua vizuri, baadhi yao wana uwezo mkubwa kushinda hata sisi tuliobaki huku ila tu tunachowashinda sisi ni uzoefu lakini wakiamua kupambana ushindi utapa­tikana na ninaamini itakuwa hivyo,” alisema Tambwe ambaye amewahi kutamba na Simba.


No comments:

Post a Comment