Thursday, 1 February 2018

Emmanuel Okwi afunguka mambo ambayo Simba inayotakiwa kufanya.

Image result for Emmanuel Okwi
Mshambuliaji wa Simba, Emmanuel Okwi amesema pamoja na Simba kuendelea kuongoza lakini bado wana kazi ngumu kutokana na ushindani wa ligi ulivyo.

Simba inaongoza Ligi Kuu Bara kwa tofauti ya pointi tano tofauti ya Azam FC wanaoshika nafasi ya pili.

Okwi amesema wanaamini wako katika nafasi nzuri lakini lazima wafanye juhudi zaidi.

“Tunaongoza ligi kwa sasa, lakini utaona tofauti ni ndogo sana na anayetufuatia. Maana yake kama timu tunatakiwa kuendelea kupambana hadi mwisho.

“Ushindani ni mkali sana, kila timu inataka kufanya vizuri na sisi tunataka kufanya vizuri. Tumekuwa tukijituma kama timu kwa faida ya klabu yetu na tunajua bado tunatakiwa kujituma,” alisema.

Okwi ndiye anayeongoza kwa ufungaji wa mabao katika Ligi Kuu Bara akiwa na 12.

Mara nyingi anapohojiwa Okwi amesema kitu cha kwanza kwake ni timu kwa kuwa kama mchezaji yeye na wenzake wamekuwa wakipigana kwa ajili ya timu.

No comments:

Post a Comment