Monday 12 February 2018

Jose Mourinho aeleza kilichojificha kuhusu sababu ya kufungwa na Newcastle.

Image result for Jose Mourinho vs newcastle
Meneja wa Manchester United Jose Mourinho amesema kuwa klabu yake haingefunga bao hata kama ingecheza kwa saa kumi baada ya upande wake kupoteza kwa bao 1-0 dhidi ya Newcastle.


Bao la dakika ya 65 la Matt Ritchie lilisababisha The Red Devils kushindwa kwa mara ya tano msimu huu.
Sasa Manchestrer United wako nyuma ya viongozi Manchester City kwa pointi 16.
"Miungu yao ya kandanda ilikuwa wazi nao," alisema Mourinho. "Haingewezekana leo."
Meneja huyo wa zamani wa Chelsea alisema kuwa Newcastle walicheza kama wanyama kushinda nyumbani kwa mara ya kwanza tangu Oktoba.
"Hisia zangu ni kuwa tungecheza kwa saa 10 na hatungefuga bao," alisema.

No comments:

Post a Comment