Sunday 11 February 2018

Kocha wa Simba aeleza anachokitaka Simba wawafanyie Gendamarie Leo.

Image result for kocha wa Pierre Lechantre
Kikosi cha Simba kitashambulia mfululizo na kwa kasi kubwa katika mechi yao dhidi ya Gendamarie kutoka Djibouti.

Taarifa kutoka ndani ya Simba zinaeleza, Kocha Mkuu, Pierre Lechantre amewataka wachezaji wake kucheza kwa kasi na kushambulia mfulilizo ili kupata mabao ya haraka.

Mechi hiyo ya Kombe la Shirikisho Afrika, inapigwa leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

“Kocha anataka kushambulia na kupata mabao, amewaeleza wachezaji mengi lakini kikubwa ni umakini katika umaliziaji,” kilieleza chanzo.

Kocha huyo alikaa na wachezaji wake na kutumia zaidi ya nusu saa akiwaeleza kinachotakiwa kufanyika katika mechi hiyo ya Gendamarie ambao wanaonekana ni dhaifu.


Hata hivyo, kocha huyo inaelezwa amewasisitiza kutotanguliza dharau na kuhakikisha wanashinda kwa mabao idadi nzuri.

No comments:

Post a Comment