Thursday, 1 February 2018

Kocha wa Simba Perre Lechantre awaandalia Ruvu Shooting dozi yao.

Image result for Kocha Mkuu wa Simba, Pierre Lechantre AANZA MAZOEZI
Kocha Mkuu wa Simba, Perre Lechantre atakiongoza kikosi chake katika mazoezi leo kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

Simba inafanya maandalizi yake kabla ya kuivaa Ruvu Shooting katika mechi ya Ligi Kuu Bara, Jumapili.

Kikosi cha Simba kimekuwa na mwendo mzuri kwani ndani ya mechi nne za ligi kimeshinda zote kwa jumla ya mabao 12.

Lechantre ameiongoza Simba katika mechi moja na kuiwezesha kushinda mabao 4-0 dhidi ya Majimaji.

No comments:

Post a Comment