Monday, 19 March 2018

Rais wa TFF afichua ishu ya Wambura asema sitacheka na mtu hata kama ni rafiki yangu.

Related image
Kauli 5 alizozisema Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Wallace Karia, wakati akizungumza na Wahariri wa Michezo katika Hotel ya SeaScape, Kunduchi, Dar es Salaam. 


"Nitasimamia na kupambana na mtu yeyote atakayeleta mchezo na masuala ya fedha. Kiongozi mmoja alijaribu kucheza na mapato ya uwanjani, Kamati imefanya kazi yake kafungiwa. Mimi sitacheka na mtu hata kama ni rafiki yangu kama asipokua muadilifu".

"Matumizi mabaya ya fedha Uongozi uliopita, umepelekeea FIFA kutunyima fedha za uendeshaji $700,000 kwa kipindi cha miaka minne sasa tangu 2014. Tumeongea na Infantino amekubali tutelekeze mapungufu yaliyokuwepo na yuko tayari kutupatia fedha hizo kwa mkupuo".

"Kuna Kamati za TFF ambazo viongozi wake Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti ni lazima wawe Wajumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF".

"Kamati Huru ni Kamati za Kisheria, Kamati ya Nidhamu, Kamati ya Rufaa ya Nidhamu, Kamati ya Maadili, Kamati ya Rufaa ya Maadili".

"Viongozi wa kamati hizi ni Wenyeviti na Makamu wake ni viongozo huru ambao sio wajumbe wa Kamati ya Utendaji TFF".


No comments:

Post a Comment