Kiungo wa kati wa Chelsea na Ufaransa N'Golo Kante, 26, ni miongoni mwa wachezaji ambao Paris St-Germain inapanga kujaribu kuwanunua mwisho wa msimu. (Canal + kupitia Goal.com)
Mshambuliaji Mjerumani wa RB Leipzig wa miaka 22 Timo Werner amewaambia Liverpool na Manchester United wasiwe na matumaini ya kumchukua mwisho wa msimu. (Mirror)
Fowadi wa Atletico Madrid Antoine Griezmann, 26, naye anadaiwa kuanza kutafuta nyumba eneo la Catalonia katika kinachoaminika kwamba ni maandalizi yake akitarajia uwezekano wake wa kuhamia Barcelona. (Marca)
Lakini meneja wa Atletico Diego Simeone amepuuzilia mbali uvumi kuhusu uwezekano wa Mfaransa huyo kuhama karibuni (Goal.com)
Juventus wako tayari kutoamua kuhusu kiungo wa kati wa Liverpool Emre Can hadi mwisho wa msimu. Mjerumani huyo wa miaka 24 atamaliza kutumikia mkataba wake wa sasa Anfield Julai na anaweza kujiunga na miamba hao wa Italia bila ada yoyote wakati huo. (Liverpool Echo)
Arsenal wanakabiliwa na ushindani kutoka kwa Napoli na Roma katika juhudi zao za kutaka saini ya kipa Mfaransa Alban Lafont mwenye miaka 19 ambaye anachezea Toulouse. (L'Equipe - kwa Kifaransa)
Kiungo wa kati wa Barcelona na Croatia Ivan Rakitic, 30, amesema klabu hiyo inaweza kumpokea kwa mikono yote miwili mshambuliaji wa Brazil Neymar aliyehamia Paris St-Germain. Hii ni baada ya taarifa kuzokeza kwamba Mbrazil huyo wa miaka 26 anataka kuihama klabu hiyo Ligue 1 side. (ESPN)
Meneja wa West Brom Alan Pardew anatarajiwa kufanya mazungumzo na wamiliki wa klabu hiyo leo Jumatatu kuamua iwapo ataendelea kusalia kazini. (Guardian)
Kipa wa West Brom Ben Foster amesema anasikitika sana kuhusu hali ya Pardew uwanjani The Hawthorns. (Express & Star)
Wamiliki wa West Ham wameitisha mazungumzo ya lazima na meya wa London Sadiq Khan na kusema kwamba hawatalazimishwa kuwazuia mashabiki kuhudhuria mechi uwanja wao wa London. (Mirror)
Mmiliki mwenza wa West Ham David Gold aliachwa na majonzi baada ya fujo za mashabiki wakati wa mechi yao dhidi ya Burnley mnamo Jumamosi. (Sky Sports)
Nahodha wa West Ham Mark Noble huenda asiadhibiwe hata baada yake kuonekana akikabiliana na shabiki aliyekuwa ameingia uwanjani wakati wa mechi. (Mail)
Mreno anayechezea Monaco Rony Lopes, 22, amesema angependa kurejea Manchester City siku za usoni. Aliihama klabu hiyo 2015. (Manchester Evening News)
Meneja wa Sunderland Chris Coleman amesema alilazimika kubahatisha kuhusu wachezaji walionunuliwa na klabu hiyo mwezi Januari baada ya klabu hiyo kuendelea kutatizika hata baada yao kuwasili Stadium of Light. (Sunderland Echo)
Meneja wa Newcastle Rafael Benitez atatathmini upya mustakabali wa mshambuliaji wa Serbia Aleksandar Mitrovic katika klabu hiyo mwezi Mei. Hii ni baada ya mchezaji huyo wa miaka 23 kung'aa sana akiwa kwa mkopo katika klabu ya Fulham inayocheza ligi Championship. (Newcastle Chronicle)
Bora zaidi kutoka Jumapili
Liverpool wana imani kwamba wataweza kumpata kipa wa England na Stoke Jack Butland mwenye miaka 24 kwa uhamisho wa £40m utakaovunja rekodi. (Sunday Mirror)
Manchester United wanapata kumnyatia beki wa kushoto anayechezea Juventus Alex Sandro, 27, mwisho wa msimu. Mbrazil huyo anatarajiwa kununuliwa kwa mkataba ambao utahusisha beki Mwitaliano Matteo Darmian, 28, akihamia Italia. (Sunday People)
Paris St-Germain hawana mpango wowote wa kumwuza mshambuliaji wao Neymar, 26, kwa klabu yake ya zamani Barcelona au mahasimu wao Real Madrid. (Sky Sports)
AC Milan wanatarajiwa kuwasilisha ombi la kumchukua kiungo wa kati wa Arsenal Jack Wilshere, 26, ambaye atakuwa bila mkataba mwisho wa msimu. Wilshere kufikia sasa hajaafikiana na klabu hiyo kuhusu mkataba mpya. (Sunday Express)
Meneja wa Manchester City Pep Guardiola, 47, amesema anapanga kuendelea kuwa mkufunzi kwa miaka 10. Guardiola anafanya mazungumzo na City kuhusu uwezekano wake wa kuongeza mkataba wake wa sasa ambao unamalizika 2019. (Sunday Mirror)
Real Madrid watajaribu kumchukua kipa wa Hajduk Split kutoka Croatia Karlo Letica mwenye miaka 21 iwapo watashindwa kunyakua nyota wa Manchester United David de Gea, 27, au Mbelgiji anayelinda ngome ya Thibaut Courtois, 25. (Marca)
No comments:
Post a Comment