Friday 13 April 2018

Jamhuri Kihwelo afuguka anachokiona kuhusu ishu ya Yanga na Lwandamina..

Image result for Jamhuri Kihwelo
Kocha wa Dodoma FC, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ amefunguka kuwa kuondoka kwa Mzambia George Lwandamina aliyekuwa kocha mkuu wa timu hiyo, ni pigo na huenda ikawaathiri wachezaji kisaikolojia kutokana na michuano iliyopo mbele yao.

Hivi karibuni, Lwandamina aliondoka Yanga na kwenda kuingia mkataba na klabu ya nchini kwao, Zesco United ambayo alikuwa akiifundisha kabla ya kutua hapa nchini.

Julio alisema kuwa kuondoka kwa kocha huyo ni pigo kwa Yanga hasa kutokana na hali ambayo inapitia timu hiyo kwa sasa. 

Julio alisema kuondoka kwa Lwandamina huenda kukawaathiri wachezaji kisaikolojia na bado wakiwa na majukumu mazito mbele yao.

“Yanga ni timu inayopambana msimu huu lakini kitendo cha Kocha Lwandamina kuondoka na timu ikiwa inamhitaji ni pigo sababu wana michuano mikubwa mbele yao.

“Lakini hawapaswi kukata tamaa sababu mimi ninamuamini (Shadrack) Nsajigwa ni kocha mzuri ambaye tayari amekaa na makocha hao wakubwa wenye uzoefu, hivyo anaweza kupambana na kuweza kuibeba Yanga,” alisema Julio.

No comments:

Post a Comment