Friday 13 April 2018

Ukweli kuhusu tetesi za kocha Hans van der Pluijm kutua Azam FC msimu ujao.

Image result for Hans van der Pluijm
Kuna taarifa kwamba Kocha Hans van der Pluijm ameishamalizana na Azam FC ambayo ataanza kuinoa mara tu baada ya msimu huu kwisha.

Ligi imebakiza takwibani mechi saba au nane kwa kila timu.

Inaelezwa kwamba kimyakimya Pluijm kamalizana na Azam FC.

"Kweli kocha amesaini mkataba wa miaka miwili na kila kitu safi, akimaliza msimu anaenda zake Azam FC," kilieleza chanzo.

Kwa sasa, Pluijm anainoa Singida lakini Yanga inaonekana ilipania kumpata ya kuondoka kwa Kocha George Lwandamina ambaye amerejea kwao Zambia na kujiunga na Zesco tena.

Ingawa inaonekana kocha huyo asingependa kulizungumzia suala hilo mapema sana.


No comments:

Post a Comment