Thursday 5 April 2018

Orodha ya wachezaji wa Simba watakaokosa mchezo na Mtibwa Sugar.

Related image
Kuelekea mchezo wa Ligi Kuu Bara Jumatatu ya wiki ijayo, klabu ya Simba itawakosa wachezaji kadhaa ambao wamekuwa sehemu ya kikosi cha kwanza.


Simba itawakosa Juuko Murushid, James Kotei na Erasto Nyoni ambao wamefikisha idadi ya kadi tatu za njano katika msimu huu wa ligi kuu bara.

Kwa mujibu wa sheria za soka, mchezaji anapofikisha idadi ya kadi hizo tatu, hawezi kuruhusiwa kucheza mchezo mmoja unaofuatia.

Wachezaji hao walipata kadi za njano kila mmoja katika mchezo uliopita dhidi ya Njombe Mji ambao Simba walishinda kwa mabao 2-0.

Kikosi hicho kimeweka kambi mjini Iringa hivi sasa kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wa ligi dhidi ya Mtibwa Sugar utakaopigwa Jumatatu ya wiki ijayo.



No comments:

Post a Comment