Friday 6 April 2018

Rais Magufuli kuzindua ukuta wa madini ya Tanzanite leo

Image result for rais magufuli akiwa na wanajeshi
Rais John Magufuli wa Tanzania, leo anatarajiwa kuzindua ukuta wa machimbo ya madini ya Tanzanite,iliopo eneo la Mererani, kaskazini mwa nchini Tanzania

Ukuta huo wenye urefu wa kilomita 24.5 na urefu wa mita tatu kwenda juu, umejengwa kufuatia agizo lililotolewa na Rais John Magufuli, kama jitihada za kudhibiti na kuzuia utoroshwaji wa madini hayo, ambayo yanapatikana nchini Tanzania pekee.
Rais Magufuli aliagiza kujengwa ukuta kuzunguka mgodi wa Tanzanite mwaka jana
Image captionRais Magufuli aliagiza kujengwa ukuta kuzunguka mgodi wa Tanzanite mwaka jana
Awali, Mwezi Februari, wakuu wa vyombo vya usalama, walitembelea eneo hilo, kuukagua ukuta huo uliojengwa kwa gharama za Kitanzania isiyozidi bilioni 6.
Walisisitiza kuwa lengo la kujengwa kwake ni kuzuia uhalifu na si kuwazuia wachimbaji wakubwa na wadogo kupata riziki zao.
"Waanze kujenga ukuta eneo hilo lote na kazi hii ifanyike haraka, watakapojenga ukuta wataweka kamera na patakuwa na mlango mmoja ambapo patajengwa vifaa maalum, nataka niwaeleze ukweli ndugu zangu wa Simanjiro hata kama utameza Tanzanite itaonekana" Agizo la Rais Magufuli mwaka uliopita
Image caption"Waanze kujenga ukuta eneo hilo lote na kazi hii ifanyike haraka, watakapojenga ukuta wataweka kamera na patakuwa na mlango mmoja ambapo patajengwa vifaa maalum, nataka niwaeleze ukweli ndugu zangu wa Simanjiro hata kama utameza Tanzanite itaonekana" Agizo la Rais Magufuli mwaka uliopita
Wakitoa taarifa kwa viongozi wa ulinzi, wataalamu waliojenga ukuta huo, walisema licha ya kufanikisha ujenzi huo, changamoto mbalimbali walikutana nazo ikiwemo hatari inayo ukabili ukuta huo, kutokana na wachimbaji kulipua baruti, karibu na ukuta, hivyo kusababisha hatari za kuharibika haraka.
Ugumu wengine walioupata ni uchimbaji katika maeneo yenye miamba.

No comments:

Post a Comment