Thursday 19 April 2018

Ushauri wa Haji Manara kuhusu Milioni 600 za Yanga.

Image result for Haji Manara na yanga
Mkuu wa kitengo cha Habari na Mawasiliano katika klabu ya Simba, Haji Manara, amewapongeza watani zake wa jadi, Yanga, kufuatia kuingia hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika.


Yanga imefuzu kufika hatua ya makundi baada ya kuindosha Wolaita Dicha SC kutoka Ethiopia kwa jumla ya mabao 2-1.

Ukiachana na kichapo cha bao 1-0 walichokipata jana, faida ya mabao waliyoshinda Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kwenye mechi ya mkondo wa kwanza, inawafanya kusonga mbele na kuwaondoa Dicha SC.

Manara amesema Yanga wanastahili pongezi kwa kuwa wameliwakilisha taifa vizuri, hivyo ni busara kuwapa pongezi.

Aidha, Manara ameshauri Yanga ni vema wakatumia pesa kiasi cha zaidi ya milioni 600 walizonyakuwa baada ya kutinga kuingia hatua ya makundi, kuwalipa mishahara wachezaji pamoja na madeni mengine mbalimbali wanayodaiwa.

Akizungumza na EFM leo asububi, Manara ameshauri Yanga wafanye hivyo, huku akieleza kuwa timu hiyo ina madeni kwa baadhi ya wachezaji wa kikosi cha Yanga.

Yanga inatarajiwa kuwasili leo usiku ikitokea Ethiopia, tayari kuanza maandalizi ya mchezo wa ligi kuu bara dhidi ya Tanzania Prisons.


No comments:

Post a Comment