Thursday 24 May 2018

Lipuli FC wataja dau wanalotaka kumuachia Adam Salamba.

Image result for Adam Salamba lipuli fc
Baada ya kuwabania Yanga kuwapatia mshambuliaji wao, Adam Salamba, uongozi wa Lipuli FC umetangaza kiasi cha fedha kwa klabu yoyote inayohitaji kumnyakua mchezaji huyo.


Taarifa zinaeleza kuwa Lipuli wanahitaji kiasi cha shilingi milioni 50 pekee ili kumuachia mchezaji huyo aliyekuwa kwenye fomu nzuri msimu huu.

Awali Yanga walituma maombi ya kumuhitaji Salamba kwa ajili ya kuwapiga tafu kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika, lakini yaligonga mwamba kutokana na kanuni za TFF, CAF na FIFA kutoruhusu mchezaji kucheza zaidi ya timu mbili ndani ya msimu mmoja.

Inaelezwa kuwa klabu za Simba na Azam FC ndizo zilizoweka nia ya dhati kumsajili mchezaji huyo na mazungumzo yanaendelea mpaka sasa.

Wakati huo Yanga ambao walihitaji nia ya kuwa naye bado hawajazungumza chochote mpaka sasa kama wana lengo la kumsajili au la.

No comments:

Post a Comment