Wednesday 23 May 2018

TETESI:Sababu za Simba kupanga kumbwaga Kocha wao Pierre Lechantre.

Image result for Pierre Lechantre
Taarifa zilizo chini ya kapeti zinaeleza kuwa uongozi wa klabu ya Simba umepanga kuachana na Kocha wake Mfaransa, Pierre Lechantre huku nafasi yake ikichukuliwa na Msaidizi, Mrundi, Masoud Djuma.


Simba wamefikia hatua ya kufanya maamuzi hayo ikiwa timu yao inajiandaa kuelekea Kenya kwa ajili ya mashindano ya SportPesa Super Cup inayotarajia kuanza mwezi Juni nchini Kenya.

Kwa mujibu wa taarifa za ndani kutoka kwa mabingwa huo wapya wa ligi kwa msimu wa 2017/18 zinaeleza kuwa Simba haijaridhishwa na kiwango cha Mfaransa huyo anayepokea mshahara mkubwa kuliko Makocha wote wa Ligi Kuu Bara.

Kutokana na hali hiyo uongozi umedhamiria kumpa timu Mrundi, Masoud Djuma huku ikiwa haijaelewa kama atakuwa Kocha Mkuu au ataletwa mwingine kuchukua mikoba ya Mfaransa huyo.

Hivi karibuni taarifa zilieleza kuwa Lechantre amekuwa miongoni mwa makocha waliotuma barua kwenda Cameroon akiomba nafasi ya kuinoa timu ya taifa ya nchini humo, hivyo endapo kama atafanikiwa kuipata itakuwa ni safari yake ya kuiacha Simba.

Mfaransa huyo alikuja Simba na kusaini mkataba wa miezi sita ambao unamalizika ndani ya mwezi ujao.

Lechantre alikuja Simba kuchukua mikoba ya Mcameroon, Joseph Omog, aliyefukuzwa mapema baada ya timu kuondolewa kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho mwaka jana na Green Warriors kwa bao 1-0.

No comments:

Post a Comment