Monday 6 May 2019

Matukio yote muhimu katika mapokezi ya Mwili wa Dr.Reginald Mengi.(picha+)


MWILI wa aliyekuwa Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP, Dkt. Reginald Mengi,  umewasili nchini katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam na kupokelewa na maelfu ya waombolezaji.

 Mwili huo unapelekwa kwa msafara hadi Hospitali ya Jeshi Lugalo, iliyopo Mwenge kwa ajili ya kuhifadhiwa ambapo kesho utaagwa katika Ukumbi wa Karimjee, Posta,  na kupelekwa kwao Machame kwa mazishi yatakayofanyika Alhamisi.
 Maelfu ya waombolezaji wenye nyuso za huzuni, wengi wao wamemwaga machozi wakati mwili wa mfanyabiashara huyo aliyeaga dunia usiku wa kuamkia Mei 2, 2019 Dubai katika Falme za Kiarabu, ukiwasili.
 Watu waliojipanga barabarani kuupokea pia wamejikuta wakiangua vilio kutokana na kuguswa na msiba huo mzito kwa Tanzania na Afrika.











No comments:

Post a Comment