Friday 10 May 2019

Tetesi zote za soka Ulaya Ijumaa 10.05.2019.


Kiungo wa kati wa Chelsea Eden Hazard anataka kuhamia Real Madrid haraka iwezekanavyo , lakini Chelsea haiko tayari kumuuza mchezaji huyoi wa ubelgiji mwenye umri wa miaka 28 chini ya dau la £100m. (ESPN)


Manchester United italazimika kulipa Yuro100m iwapo wanataka kumsaini mshambuliaji wa Barcelona Philippe Coutinho. Mchezaji huyo wa Brazil mwenye umri wa miaka 26 ni miongoni mwa mwachezaji 10 ambao wanatarajiwa kuondoka katika klabu hiyo mwisho wa msimu huu . (AS - in Spanish)


Mkufunzi wa Manchester City Pep Guardiola amepunguza hamu yake ya kutaka kumsaini mshambuliaji wa Sporting Lisbon, 24 na Ureno Bruno Fernandes. (The Sun)

Hatahivyo Manchester United wana hamu ya Fernandes, huku mkufunzi Ole Gunnar Solskjaer akitaka kuimarisha safu yake ya kati . (ESPN)

Beki wa Tottenham Toby Alderweireld anasema kwamba yuko asilimia 100 kwamba atarudi kujiunga na Ajax siku zijazo. Raia huyo wa Ubelgiji ,30, alihudumu katika klabu hiyo ya Uholanzi kutoka 2008 hadi 2013. (Voetbal International via Sky Sports)

Atletico Madrid lazima iamue iwapo italipa dau jingine la Yuro 18m kwa Chelsea ili kumsaini mshambuliaji wa Uhispania Alvaro Morata kwa mkopo kwa msimu mmoja zaidi . (AS - in Spanish)

Beki wa Tottenham na Uingereza Danny Rose anasema kuwa ataondoka katika klabu hiyo vyema iwapo fainali ya kombe la mabingwa Ulaya itakuwa mechi yake ya mwisho na Spurs. Rose mwenye umri wa miaka 28 aliongeza kwamba anahisi kwamba atauzwa (Mirror)

Nahodha wa Ajax na beki Matthijs de Ligt, 19, ataelekea Uingereza au Uhispania mwisho wa msimu, kulingana na afisa mkuu mtendaji wa klabu hiyo Edwin van der Sar. Raia huyo wa Uholanzi amehusishwa na uhamisho wa Barcelona. (Sky Sports)

Klabu mpya iliopandishwa katika ligi kuu ya Uingereza Sheffield United inamtaka mshambuliaji wa Middlesbrough ,26, raia wa DRC Britt Assombalonga. (Northern Echo)

Chelsea inatumai kufufua mradi huo ili kupanua uwanja wa Stamford Bridge kupitia kupunguza gharama kutoka £1bn hadi £500m (New Civil Engineer)

Beki wa Tottenham Jan Vertonghen hajulikani iwapo atacheza fainali ya ligi ya mabingwa dhidi ya Liverpool. Raia huyo wa Ubelgiji mwenye umri wa miaka 32, alipata jeraha katika mguu wake katika dakika za mwisho za ushindi wa Spurs dhdi ya Ajax (Guardian)

No comments:

Post a Comment