POLISI nchini Rwanda leo Februari 17, 2020, imetangaza kifo cha mwanamuziki mashuhuri nchini humo, Kizito Mihigo (38), ambaye inadai kuwa amefariki dunia kwa kujinyonga alipokuwa akizuiliwa kwenye kituo kimoja cha polisi mjini Kigali.
Habari za kufariki dunia kwa kujinyonga kwa mwanamuziki huyu aliyegeuka kuwa mwanasiasa zimefahamika asubuhi. Kizito alikuwa amekaa siku tatu kwenye kizuizi cha polisi baada ya kukamatwa kwenye kile polisi walichodai ni jaribio la kutorokea nchini Burundi kupitia upande wa kusini mwa nchi ili kujiunga na makundi yenye silaha.
Mwanamuziki huyu kwa mara ya kwanza alikamatwa mwaka 2015 na kuhukumiwa kifungo cha miaka kumi jela baada ya kupatikana na hatia ya kushirikiana na makundi yenye silaha yaliyokuwa na nia ya kuipindua serikali ya Rwanda.
Baadhi ya wadadisi wamekuwa na maoni kuhusu kifo cha mwanamuzi huyu.
Hata hivyo, kitendawili ni kwamba tangazo la polisi pia limesema amejiua siku mbili baada ya marafiki na jamaa zake kumtembelea kwenye kituo hicho cha polisi.
Watu wanahoji usalama wa vituo vya polisi kwa mahabusu kwa kuzingatia kila mahabusu anayeingia hupekuliwa na vitu vyote kusalia nje.
Hilo ni swali ambalo lingejibiwa na msemaji wa jeshi la polisi, John Bosco Kabera, ambaye hakuweza kupatikana na mara moja.
Chanzo: Sylivanus Karemera/DW Kigali
No comments:
Post a Comment