Shirika la afya duniani limesema dunia inapaswa kujiandaa kwa uwezekano wa janga la virusi vya corona.
WHO linasema ni mapema sana kuuita mlipuko wa virusi hivyo janga lakini nchi zinapaswa kuwa katika "awamu ya maandalizi".
Janga ni pale maambukizi ya ugonjwa yanaposambaa kwa urahisi kutoka kwa mtu mmoja hadi mwingine katika maeneo mengi ya dunia.
Visa zaidi vya virusi ambavyo husababisha ugonjwa kupumua Covid-19, vinaendela kujitokeza, huku milipuko ya ugonjwa huo ikibainika katika mataifa ya Korea Kusini, Italia na Iran ikisababisha.
Mkuu wa WHO Tedros Adhanom Ghebreyesus aliwaambia waandishi wa habari Jumatatu kwamba idadi ya visa vya Corona katika siku za hivi karibuni katika mataifa ya Iran, Italia na Korea Kusini vina "tisha sana''.
Hata hivyo aliongeza kuwa : "Kwa sasa hatushuhudii kiwango kibaya cha ugonjwa au vifo.
" Je ugonjwa huu una uwezekano wa kuwa janga? Kabisa, unaweza. Je bado haujawa kutokana na tathmini yetu? Kutokana na tathmini yetu, bado haujawa."
'Ujumbe muhimu ambao unaweza kutoa matumaini kwa nchi, kutia moyo na kuzipa guvu ni kwamba virusi hivi vinaweza kudhibitiwa, kusema ukweli kuna nchi nyingi ambazo zimefanya hilo ," alisema Bw.
"Kutumia neno 'janga' kwa sasa haifai kwasababu ukweli ni kwamba inaweza kusababisha hofu."
Lakini Mike Ryan mkuu wa mpango wa dharura wa afya wa WHO ,amesema sasa ni muda wa "kufanya kila liwezekanalo kujiandaa kwa janga ".
No comments:
Post a Comment