Friday 1 May 2020

Tetesi za Soka Ulaya Ijumaa 01.05.2020


Real Madrid na Barcelona wamejiunga na kinyang'anyiro cha kumsajili winga wa Borussia Dortmund na England Jadon Sancho. Manchester United pia wako mbioni kumsaka nyota huyo wa miaka 20-year-old. (Bild - in German)

Manchester United inapigiwa upatu kumnunu kiungo wa kati wa Aston Villa midfielder Jack Grealish, 24, kuliko mchezaji mwenza wa England na Leicester James Maddison, 23. (Manchester Evening News)

Mipango ya kurudi kwa EPL kushika kasi wiki hiiTetesi za soka Ulaya Alhamisi 30.04.2020

Arsenal inakabiliwa na ushindani kutoka kwa AC Milan kumsajili kiungo wa kati wa Real Betis na Ufaransa Nabil Fekir, 26. (Marca - in Spanish)
Bayern Munich wako tayari kulipa £60m tu kumnunua winga wa Manchester City na Ujerumani Leroy Sane, 24. (Sky Sports)

Barcelona haitamuuza winga wa Brazil Philippe Coutinho kwa bei ya chini ya euro milioni 100 sawa na (£87m). Chelsea wamehusishwa na kiungo huyo matata wa miaka 27. (Mundo Deportivo - in Spanish)
Kiungo wa kati wa Brazil Fernandinho, 34, anataka kusaini mkataba mpya Manchester City. (Sky Sports)

Winga wa Bournemouth na Scotland Ryan Fraser, 26, anataka kujiunga na Tottenham mkataba wake utakapomalizika msimu huu. (Football Insider)

Manchester United huenda isikubali ofa yoyote ya kumuuza kipa wake Dean Henderson, 23, dirisha la uhamisho litakapofunguliwa. Kipa huyo Muingereza kwa sasa yuko Sheffield United. (ESPN)

No comments:

Post a Comment