Sunday 18 October 2020

KENYA YATANGAZA IDADI MPYA YA WAGONJWA WA VIRUS VYA CORONA.


Wizara ya Afya nchini Kenya

imethibitisha watu 685 kuambukizwa

#Coronavirus ndani ya saa 24 huku idadi

jumla ya walioambukizwa kufikia sasa

ikiwa 44,881

Watu 635 ni raia wa Kenya huku 50

wakiwa raia wa kigeni. Wanaume ni 456

na wanawake 229. Watu hao wana umri

kati ya mwaka mmoja hadi tisini na tisa

Wizara imebainisha kuwa idadi

ya

wagonjwa wanaopelekwa katika vyumba

vya wagonjwa mahututi imefikia 28

Kwa maelezo hayo, Wizara imesema bila

shaka hilo ni wimbi la pili la #Coronavirus.

Imetahadharisha kwamba wananchi

wasipofuata kanuni zilizowekwa hali

huenda ikawa mbaya zaidi

No comments:

Post a Comment