Monday 19 October 2020

Tetesi za soka Ulaya



 Kocha wa Barcelona Ronald Koeman anataka kumuongeza mshambuliaji wa Lyon na uholanzi Memphis Depay, 26, katika kikosi chake Januari. (AD, via Goal)

kiungo wa kati wa Liverpool na Uholanzi Georginio Wijnaldum, pia analengwa na Barcelona. Mchezaji huyo, 29, yuko mwaka wa mwisho wa mkataba wake na msimu ujao atakuwa huru. (AD, via Sky Sports)

.Manchester United ina nia ya kumsajili kiungo wa kati wa Real Madrid na Uruguay Federico Valverde, 22, na inaweza kutumia kiungo wao wa kati mshindi wa kombe la dunia kwa Ufaransa, Paul Pogba, 27, katika makubaliano ya mabadilishano. (Sun)

Ronald Koeman pia ameisihi bodi ya Barcelona kukamilisha uhamisho wa mlinzi wa Manchester City na Uhispania Eric Garcia, 19, Januari. (Mirror)

Kocha wa West Ham David Moyes anasema alikuwa na helikopta tayari kumchukua juu kwa juu Gareth Bale aliyetoka Tottenham na kuelekea Real Madrid mwaka 2013 wakati huo akiwa kocha wa Manchester United. Mshambuliaji huyo wa Wales, 31, hivi karibuni alirejea Spurs kwa mkopo. (Mail)

Msambuliaji wa Manchester United na England Marcus Rashford, 22, amesema siku ya mwisho ya kuwasili kwa mshambuliaji wa Uruguay Edinson Cavani, 33, kutasidia klabu hiyo kushindania kombe. (Sky Sports)

No comments:

Post a Comment