Monday 23 August 2021

Simba, Yanga Mziki Umekamilika Kuelekea Ngao ya Jamii Septemba 25


HAKUNA kisingizio Septemba 25, mwaka huu kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii ambao utakuwa ni ufunguo wa msimu wa 2021/22 hapa nchini ambapo Simba SC watacheza dhidi ya Yanga SC.


Utamu wa mchezo huo 
utakaochezwa Uwanjawa Mkapa, Dar, unazidi kuongezeka kutokana na timu zote kuonekekana kuimarika zaidi kutokana na usajili ambao umefanywa hadi sasa.

 

Msimu uliopita, Yanga waliteswa sana eneo laushambuliaji ndiyo maana kwenye dirisha hili la usajili wamecheza zaidi kwenye eneo hilo kwa kusajili nyota ambao wanaamini wataletamabadiliko.

 

Kwa usajili wa timu zote ambao umefanyika hadi sasa, Yanga wanaonekana kuimarika zaidi kwenye eneo la mbele wakiwa na maingizo mapya, Fiston Mayele, HeritierMakambo, Jesus Moloko na Dickson Ambundo.Nyota hao wanakwenda kuungana na nyota kama Deus Kaseke, Ditram Nchimbi na Yacouba Songne.

Wakati Yanga wakitamba na washambuliaji zaidi, Simba wao hawakuwa na shida sanakwenye eneo hilo baada ya kuwepo nyota kama John Bocco, Chris Mugalu na MeddieKagere.

 

Wao wakaamua kucheza na viungo, wakimleta Peter Banda, Duncan Nyoni, Pape Ousmane Sakho, Abdulswamad Kassim na Sadio Kanoute ambao wanakwenda kuungana na Tadeo Lwanga, Jonas Mkude,Said Ndemla, Mzamiru Yassin, Hassan Dilunga na Rally Bwalya.

 

Ukiachana na timu zote kutamba na usajili wao huo, imebainika vikosi vyao vimekuwa vipana zaidi na hatari.

 

Kwa upande wa Yanga, kikosi chao cha kwanza chini ya Kocha Nadreddine Nabi,kinatarajiwa kuwa hivi; Diarra Djigui, Djuma Shabani, David Bryson, Bangala Litombo,Bakari Mwamnyeto, Mukoko Tonombe, Feisal Salum, Khalid Aucho, Heriter Makambo,Fiston Mayele na Yacouba Songne.

 


Kikosi cha pili cha Yanga 
kinatarajiwa kuwa na nyota hawa, Erick Johora, KibwanaShomari, Yasin Mustapha, Abdallah Shaibu, Dickson Job, Zawadi Mauya, Ducapel Moloko, Deus Kaseke, Yusuph Athumani, Saidi Ntibazonkiza na Dickson Ambundo.

 

Wakati vikosi hivyo viwili vikikamilika, nyota wengine watakuwa wakisubiri ambao niRamadhani Kabwili, Adeyum Salehe, Balama Mapinduzi, Paul Godfrey, Farid Mussa naDitram Nchimbi.

 

Kwa upande wa Simba, kikosi chao cha kwanza kinatarajiwa kuwa hivi; Aishi Manula,Shomari Kapombe, Mohammed Hussein, Henock Baka, Joash Onyango, Taddeo Lwanga, Peter Banda, Rally Bwalya, Chris Mugalu, John Bocco na Pape Ousmane Sakho.

 

Kikosi cha pili cha Simba kinatarajiwa kuwa hivi; Beno Kakolanya, Israel Mwenda, Gadiel Michael, Erasto Nyoni, Pascal Wawa, Jonas Mkude, Bernard Morrison, Sadio Kanoute, Meddie Kagere, Yusuph Mhilu na Duncan 
Nyoni.

 

Wanaobaki ni Perfect Chikwende, Hassan Dilunga, Said Ndemla, Abdulswamad Kassim, Mzamiru Yassin, Ibrahim Ame, sambamba na Jeremia Kisubi na Kibu Denis ambao wanatajwa kila mmoja kusaini mkataba wamiaka miwili ingawa bado hawajatangazwa rasmi.

No comments:

Post a Comment