Katika mkutano wa kuhitimisha kampeni za kugombea urais wa chama
cha mapinduzi uliohudhuriwa na halaiki ya wakazi wa jiji la Mwanza na
viunga vyake kwanza rais Kikwete anatoa onyo kwa wale waliodhamiria
kufanya fujo siku ya upigaji kura.
Pia Dr.Kikwete anachukua fursa hiyo kukana kuhusika kwake katika
sakata la Richmond huku akidai kuwa kanuni na taratibu za kupatikana kwa
kampuni hiyo zilikiukwa.
Mgombea mwenza wa chama hicho Samia Hassani Suluhu anaueleza umati
wa watanzania waliohudhuiria mkutano huo juu ya kero ya upatikanaji wa
maji katika maeneo alikozunguka na kuahidi kulipatia ufumbuzi.
Mgombea wa kiti cha urais Dr.John Pombe Magufuli ambaye amelitikisa
jiji la Mwanza na kuvunja rekodi ya mahudhurio katika mkutano huo kwa
upande wake ameonesha kukerwa na suala la mgao wa umeme na kuahidi
kulitatua na kuto onyo kwa wale wanaohujumu upatikanaji wa umeme.
Aidha mbali na kugusia takribani sekta zote kero kwa wananchi pia
ameahidi kufufua viwanda vilivyokufa ili kutoa fursa kwa vijana na
kuwataka waliobinafsishiwa na kuvitelekeza wanavifufua.
Takribani siku 60 za kuomba kura kwa watanzania zimekamilika na
sasa wananchi watafanya maamuzi kupitia sanduku la kura kumuweka
madarakani kiongozi walioridhishwa na sera zake jumapili ya October 25
ya mwaka huu.
No comments:
Post a Comment