Saturday 24 October 2015

UKAWA WAFUNGA KAMPENI ZAO LEO JANGWANI

Umoja wa katiba ya wananchi ukawa umehitimisha kampeni zake katika viwanja vya Jangwani Jijini Dar es Salaam  ambapo mwenyekiti wa taifa wa chama cha demokrasia na maendeleo chadema Mh.Freeman Mbowe amesema ushindi ni lazima.

















Akihutubia maelfu ya wanachama wa chama hicho Mh.Mbowe amesema ushindi ni lazima na hivyo amewataka wananchi kushangilia  ushindi.
Naye mgombea urais kwa tiketi ya chadema Mh.Edward Lowassa  amesema  safari ya kampeni ilikuwa ngumu na yenye changamoto nyingi lakini jambo jema zimeisha salama kikubwa watu wajitokeza kwenda kupiga kura.
 
                          Edward lowasa

Akitoa salamu zake mgombea urais visiwani Zanzibar kwa tiketi cha chama cha wananchi CUF Mh.Seif Sharif Hamad amesema wazanzibar wamejipanga vyema na wamesema watamchagua  Lowassa naye mgombea mwenza Mh.Juma Duni Haji amewataka wananchi kulinda kura zao.
 
               Mgombea wa uraisi Zanzibar Sharif Hamad

Akitoa salamau zake mzee Kingunge Ngombare Mwiru amesema CCM imechoka na kwa upande wake Mh.James Mbati mwenyekiti mwen za UKAWA amesema ni bora CCM ikubali kuachia madaraka kwa amani bila ya vurugu.
 
 
 
 

No comments:

Post a Comment