Saturday 21 November 2015

Bi Anne Waiguru waziri mwenye ushawishi mkubwa nchini kenya ajiuzulu kwa tuhuma za ufisadi








Waiguru 















Waziri mwenye ushawishi mkubwa katika serikali ya Rais Uhuru Kenyatta amejiuzulu wadhifa wake baada ya shinikizo kutolewa ajiuzulu kutokana na tuhuma za ufisadi.
Bi Anne Waiguru, ambaye amekuwa Waziri wa Mipango na Ugatuzi, ameambia wanahabari Nairobi kwamba ameshauriwa na daktari wake “achukue muda kupumzika”.
Amewaambia wanahabari kwamba amemwandikia Rais Kenyatta akimtaka amuondolee majukumu yake.
Hata hivyo amesisitiza kwamba hana hatia.
“Ninafuata ushauri wa daktari na nimemuomba Rais aniondolee majukumu yangu kama waziri ... na akiona inafaa, anipe majukumu ambayo si mazito,” Bi Waiguru amesema

No comments:

Post a Comment