Tuesday 10 November 2015

David Moyes Atimuliwa Real sociedad



 Kocha wa Timu ya Real sociedad David Moyes atimuliwa na timu hiyo matokeo na maendeleo ya Timu hiyo kutoridhisha

                         David Moyes
Mkufunzi huyo wa umri wa miaka 52 aliongoza klabu hiyo kumaliza nambari 12 msimu uliopita baada ya kuchukua usukani manmo Novemba 10, 2014.
Real Sociedad iko karibu sana na eneo la kushushwa ngazi, ikiwa juu kutokana na wingi wa mabao baada ya kulazwa 2-0 Ijumaa ugenini na klabu iliyopandishwa ngazi msimu huu Las Palmas. Hiyo ni mechi yao ya nne kushindwa katika mechi tano katika La liga. Moyes alijiunga na Sociedad baada ya kufutwa kazi katika klabu ya Ligi Kuu ya Kandada ya England, Manchester United
Taarifa kutoka kwa Sociedad imesema klabu hiyo imeamua kukatiza mkataba wa Moyes. Kocha wa zamani wa Celta Vigo na BARCELONA B Eusebio Sacristan mwenye umri wa miaka 51 amechukua usukani na ataiongoza klabu hiyo hadi mwisho wa msimu huu.

           Kocha mpya wa Real Sociedad Celta  deVigo
 Klabu hiyo kwa sasa himo nambari 16 ligini na itakutana na washindi wa Europa League Sevilla na mabingwa wa Ulaya Barcelona mechi mbili zijazo La Liga baada ya mapumziko ya kimataifa.

No comments:

Post a Comment