Tuesday 10 November 2015

Ivory Cost yaanza safari ya kucheza Kombe la Dunia

  

\Wakati ligi kuu za kandanda Ulaya zikienda mapumziko kwa ajili ya michuano ya kimataifa, Ivory cost na Ghana zitaanzisha kampeni zao za kushiriki katika Kombe la Dunia la FIFA kwa mara yao ya nne mfululizo

                               Kikosi cha Ivory Cost
 Timu hizo zina mechi za ugenini dhidi ya wapinzani wanaoorodheshwa chini yao katika viwango vya FIFA, Liberia na Comoros.
Nigeria watafunga safari kumenyana na na Swaziland ambapo kocha Sunday Oliseh amewaita kikosini Alex Iwobi wa Arsenal na Kelechi Iheanacho wa Manchester City. Aidha mshambulizi wa muda mrefu Obafemi Martins pia amerejea kwenye timu baada ya Emmanuel Emenike kustaafu.
Afrika Kusini watachuana ugenini dhidi ya Angola waati Cameroon ambao wanashikilia rekodi ya Afrika ya kucheza mara saba katika Kombe la Dunia wakipambana na Niger. Benin watashuka dimbani dhidi ya Burkina Faso wakati Morocco ambao wamefuzu mara nne wakitoana jasho na Guinea ya Ikweta. Cote d'Ivoire ambayo itakosa huduma za Yaya Toure itapambana na Liberia. Michuano hiyo inachezwa kesho na Jumatano

No comments:

Post a Comment