Rais wa Shirikisho la Kandanda la Ujerumani - DFB Wolfgang Niersbach amesalimu amri na kujiuzulu kutokana na kashfa ya malipo yaliyotolewa kwa Shirikisho la Kandanda Duniani - FIFA kuhusiana na Kombe la Dunia 2006
Mkuu wa Shirikisho la kandanda la Ujerumani – DFB Wolfgang Niersbach anakabiliwa na maswali magumu katika mkutano wa dharura kuhusiana na madai kuwa hongo ilitolewa ili Ujerumani kuandaa Kombe la Dunia la FIFA 2006.
Niersbach alifika leo kwenye kikao cha kuulizwa maswali na maafisa wa kandanda wa Ujerumani na marais wa mashirikisho 16 ya kikanda wanachama wa DFB mjini Frankfurt.
Nersbach anakanusha madai yaliyofichuliwa na jarida la Der Spiegel kuwa kombe la dunia lilinunuliwa akisema hapakuwa na hazina yoyote maalum wala kununuliwa kura. Badala yake alisema fedha hizo zilitumiwa ili kupata ufadhili wa euro milioni 170 kutoka kwa FIFA.
Mapema wiki hii polisi walivamia makao makuu ya DFB pamoja na makazi ya kibinafsi ya viongozi watatu wanaotuhumiwa katika kashfa hiyo, rais huyo wa DFB, rais wa zamani wa DFB Theo Zwanziger na katibu mkuu wa zamani wa DFB Horst Schmidt. Waendesha mashtaka pia wameanzisha uchunguzi wa madai ya kukwepa kulipa kodi dhidi yao.
No comments:
Post a Comment