Thursday, 26 November 2015

Papa francis-Familia ndio msingi wa Amani



Papa Francis ameongoza ibada ya misa ambayo imehudhuriwa na maelfu ya watu uwanja wa Chuo Kikuu cha Nairobi ambapo amesisitiza umuhimu wa familia katika jamii.Awali katika mkutano na viongozi wa dini mbalimbali, alisema dini haifai kutumiwa kuvuruga akisema “Mungu ni Mungu wa amani.”
"Jina lake takatifu halifai kutumiwa kutetea chuki na mauaji. Ninajua kwamba mashambulio ya Westgate, Chuo Kikuu cha Garissa na Mandera bado hayajasahaulika. Na sana, vijana wamekuwa wakiingizwa na kufunzwa itikadi kali kwa jina la jini kupanda woga na kuvunja umoja katika jamii,” alisema.
"Ni muhimu sana tuwe manabii wa amani, watu wa amani wanaokaribisha wengine kuishi na amani, umoja na kuheshimiana. Mungu na akaguze nyoyo za wanaohusika katika mauaji na ghasia, na azipe imani familia na jamii zetu

No comments:

Post a Comment