Tuesday 17 November 2015

Timu ya Taifa stars yashindwa kutamba katika Ardhi ya Bilda, Algeria

 Kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania 'Taifa Stars'
 Timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ imeondoshwa kwenye kinyang’anyiro cha kuwania kupangwa kwenye hatua ya makundi kwa ajili ya kutafuta nafasi ya kucheza fainali za kombe la dunia mwaka 2018 ambazo zitafanyika nchini Urusi baada ya kufungwa kwa magoli 7-0 kwenye mchezo wa marudiano uliochezwa kwenye uwanja wa Mustapher Tchaker mjini Blida, Algeria

 Stars imeondoshwa kwa jumla ya mabao 9-2 baada ya kucheza michezo miwili, mchezo wa kwanza Stars ililazimishwa sare ya kufungana kwa goli 2-2 na Algeria jijini Dar es Salaam huku mchezo wa pili uliopigwa Blida, Algeria ukimalizika kwa Stars kulala kwa goli 7-0Stars imeondoshwa kwa jumla ya mabao 9-2 baada ya kucheza michezo miwili, mchezo wa kwanza Stars ililazimishwa sare ya kufungana kwa goli 2-2 na Algeria jijini Dar es Salaam huku mchezo wa pili uliopigwa Blida, Algeria ukimalizika kwa Stars kulala kwa goli 7-0

No comments:

Post a Comment