Wednesday, 18 November 2015

Job Ndugai achaguliwa kuwa Spika wa bunge la 11 la Tanzania


                                   Job Ndugai
Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limemchagua  JOB NDUGAI kuwa SPIKA wa Bunge la kumi na moja.
 
Akitoa matokeo mara baada ya wabunge kupiga kura Katibu wa Bunge Dokta. THOMAS KASHILILA amemtaja JOB NDUGAI kuwa amepata Kura 254 ikiwa ni asilimia sabini ya kura zilizopigwa huku GOODLUCK OLE MEDEYE akipata kura 109.
Awali Katibu wa Bunge Dokta KASHILILA  alisoma Tangazo la Rais la Kuitisha Bunge na kumteua mbunge aliyetumikia kwa muda mrefu bunge la Jamhuri ya Muungano wa TANZANIA JOHN CHENGE BARIADI MAGHARIBI kuwa mwenyekiti wa muda kuongoza uchaguzi wa spika.
Wengine waliogombea nafasi hiyo ni PETER LEORNARD SARUNGI wa chama cha AFP,HASSAN KISABYA ALMASI wa NRA, RAPHAEL MALISA wa CCK, RICHARD SHEDRACK LYIMO wa TLP,ALEXENDER KISININI wa DP na HASHIM RUNGWE wa CHAUMA.
Wabunge waliosajiliwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanznaia ni 368 huku waliopiga kura za kumchagua Spika ni 354


No comments:

Post a Comment