Thursday, 26 November 2015

Utafiti mpya unaonesha ukatili wa kijinsia umeongezeka kwa ngazi ya familia

  

Utafiti uliofanywa na kitengo cha Jinsia cha chuo kikuu cha DSM hivi karibuni umeonesha kuwa ukatili wa kijinsia kwa wanawake na wasichana umeongezeka katika ngazi ya familia.
Akitoa taarifa ya utafiti huo katika mkutano wa wadau wa masuala ya jinsia makamu mkuu wa chuo hicho idara ya Taaluma Profesa FLORENS LUOGA amesema jamii inatakiwa kuachana na tamaduni zinazo wafundisha wanawake wajione kuwa chini kwenye masuala ya kijamii.
Kampeni ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia ingali ikiendelea hapa nchini na duniani kote, wadau mbalimbali wamekuwa wakikutana na kutafakari namna watakavyo wezesha jamii kupunguza na hatimae kuondokana na ukatili huo wa kijinsia

 

Kwa upande wake Mtaalamu wa masuala ya jinsia wa chuo kikuu cha DSM Profesa BERTHA KODA amesema kila mdau anatakiwa kuwajibika kwa uwezo wake katika kutafuta namna ya kumaliza ukatili wa kijinsia kwakuwa tayari serikali imekwishatunga sera na sheria lakini bado tatizo linaongezeka .
Kauli mbiu ya mwaka huu ya kupinga ukatili wa kijinsia inasema “PUNGUZA MACHUNGU YA MWANAMKE KAMA CHUNGWA TAMU, PUNGUZA UKATILI WA KIJINSIA KWA WANAWAKE”

No comments:

Post a Comment