Wednesday 9 December 2015

Desember 9 ni mwendo wa usafi tuu Magufuri awaongoza wananchi katika kuanzimisha uhuru kwa kufanya usafi

 Desember 9 kila mwaka ni siku ambayo Nchi ya Tanganyika  ambayo hivi sasa ni Tanzania ilipata uhuru mwaka 1961 chini ya muhasisi  Mwalimu Julias Kambalage Nyerere kutoka kwa waingereza
Siku hiyo imekuwa ikitumika kama kumbukumbu kwa kuanzimishwa kila mwaka kwa sherehe mbalimbali
                                   
  Raisi Dk.John Magufuri akiwa anafanya usafi maeneo ya feri jijini Dara es salaam

                                 Raisi mstaafu Dk.Jakaya kikwete na mkewe mama salma Kikwete wakionesha kuunga mkono Tamko la Rais Magufuri
Lakini kwa mwaka huu imekuwa tofauti na ilivyozoeleka mara baada ya Raisi wa awam ya Tano Dk.John Magufuri kutaka wananchi wote  kuitumia siku hii kwa kufanya usafi katika maeneo yao pamoja na mazingira  kwa ujumla hii ni katika kupiga vita baadhi ya magonjwa mbalimbali yanayosababishwa na uchafu kama kipindupindu





No comments:

Post a Comment