Wednesday, 9 December 2015

Klab ya TP mazembe yawasili nchini Japani kwa ajiri ya mashindano ya kombe la dunia la vilabu bingwa

Klabu Bingwa Afrika TP Mazembe kutoka Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo wamewasili jijini Osaka nchini Japan, kwa ajili ya michuano ya Kombe la Dunia la vilabu bingwa linaloanza kesho.
Mazembe ambao ni washindi wa CAF Klabu Bingwa Afrika, watacheza mechi ya kwanza siku ya Jumapili dhidi ya mshindi wa siku ya Alhamisi kati ya Sanfreece Hiroshima na Aukland City FC.
Miaka mitano iliyopita Mazembe waliushangaza ulimwengu kwa kuingia fainali lakini walishindwa dhidi ya Inter Milan.
Fifa wame tweet picha hii ya Mazembe wakiwasili.

No comments:

Post a Comment