Tuesday 29 December 2015

DURU za kiusalamaa nchini Pakistan zinaarifu kuwa watu 29 wameuawa na makumi ya wengine kujiruhiwa katika shambulio la kujitoa muhanga




DURU za kiusalamaa  nchini  Pakistan zinaarifu kuwa  watu 29 wameuawa na makumi ya wengine kujiruhiwa katika shambulio la kujitoa muhanga

Tukio hilo limetokea leo hii  baada  ya tukio la kujitoa muhanga, kwa kutumia  pikipiki  akilenga majengo ya  serikali katika mji wa Mardan  Kaskazini magharibi mwa Pakistani

Kamanda wa polisi wa eneo hilo faisal Shahzad amsema kuwa mtu huyo mwenye kujitoa muhanga aliripua bomu  mbele ya ofisi  ya  uhamiaji

Kwa upande wake  Daktari Ally  Khan  wa  hospitali ya eneo hilo, amesema kuwa idadi  ya watu waliojeruhiwa  imefikia  40  hadi jioni hii

Kundi la watu wanaodai  ukombozi  nchini humo limedai kuhusika na shambulio hilo, tukio ambalo linakuja sambamba na msururu wa mashambulizi kati ya  kikundi cha twalibani na makunde mengine




No comments:

Post a Comment